Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameungana na Wafanyakazi wengine duniani kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani. Watumishi hao wameshiriki sherehe za maadhimisho ya kimkoa ambayo yamefanyika katika eneo la Viwanja vya Shule ya Msingi Kakola katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga April, 01,2024.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Mhe. Anamringi Macha ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewaahidi watumishi hao kufikisha changamoto zao kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwatoa hofu Watumishi juu ya suala la Kikokotoo.Amesema kuwa ana uhakikika kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni msikivu na atalifanyia kazi.
Aidha, Mhe. Macha amesema Mhe.Rais amekuwa akiboresha mara kwa mara maslahi ya Watumishi wa Umma, pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi.
Aidha, amewataka waajiri kupeleka michango ya Watumishi wao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii suala ambalo limekuwa likilalamikiwa na Watumishi mara kwa mara na hata kuleta migogoro kwenye ulipaji wa mafao.
Kauli Mbiu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa Mwaka 2024 ni “ Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha”
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Mhe. Anamringi Macha akitoa vyeti na zawadi
kwa wafanyakazi hodari wa Halmasahuri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri Ndg. Kisena Mabuba
na Wafanyakazi Hodari.
Watumishi wa Halmashauri wakishiriki maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.