Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bwana David Rwazo pichani chini akisaini Kitabu cha wageni Shule ya Sekondari Iselamagazi mahali ambapo usaili wa Kata za Mwalukwa, Pandagichiza, Nyamalogo, Iselamagazi, Mwantini na Lyabusalu ulifanyika.
Pichani DHRO Bwana David Rwazo( Kulia) akisaini Kitau cha wageni mbele ya Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Iselamagazi.
Akizungumzia Utaratibu, DHRO huyo aliwatangazia wote waliokuja kufanya usaili kuwa wanapaswa kufata sheria na taratibu zote. na kama kuna Mtu amefanya fojari ni bora ajitowe mwenyewe kwani ni kosa la jinai kugushi cheti au taarifa zozote za Serikali.
pia Watahaniwa wote walitangaziwa kuwa kutakuwa na ukaguzi wa vyeti Halisi vyote vya Taaluma, kuzaliwa na Kitambulisho cha Nida. utaratibu ulifanyika na watahaniwa wote wenye sifa waliruhusiwa kuingia chumba cha Mtihani saa 3.30 Asubuhi na kupewa maelekezo ya ndani ya Chumba na kufika saa nne kamili Mitihani ilianza kwa kanda hiyo ya Nindo.
Kwenye Kata hizi, waliitwa wasaili wenye sifa ni 185, ila waliofanya mtihani huu wa Majaribio ni 142.
kwa muda wa saa limoja wanafunzi wote walimaliza Mitihani na kazi ya kusaisha mitihani ilianza mara moja baada ya kumaliza usaishaji na taratibu nyingine. Mkuu huyo wa Utawala alisema wanatarajia kutangaza Majina ya waliofaulu usaili huu mapema na haraka iwezekanavyo ili wapewe Mafunzo na kuanza kazi hiyo Mara Moja.
wanafunzi 142 waliwekwa kwenye Madara matatu na wasimamizi sita kwa madarasa yote Matatu.
DHRO aliatangaza kuwa utaratibu wa kuwaita Waaliofaulu au kuwajulisha wenye Kasoro utafanywa kwa njia za mawasiliano zinazoelewekwa na ni lazima matangazo hayo yawe kwenye tovuti hii ya Halmashauri. anawashauri vijana kujieusha na MATAPELI wanaotumia simu kuwapigia watu na kuwaambia kuwa wao ni Maafisa Utumishi na kuwa wanaomba hela kwa watahaniwa. Ofisi ya Mkurugenzi haihusiki na Maombi yeyote ya Pesa na watahaniwa wote wanapaswa kupeana Taarifa hii ya Matapeli.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.