Serikali imesikia kilio cha wakazi wa Kata ya Tinde na Didia kuhusu maombi yao ya
kupunguziwa bei za gharama za maji waliyokuwa wakilipa kiasi cha shilingi 2500 kwa
unit tofauti na maeneo mengine ya Shinyanga ambayo wanalipa shilingi 1400 kwa unit.
Wakazi hao sasa wataanza kulipa kiasi cha shilingi 1400 kwa unit.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro wakati wa
Mkutano wa hadhara uliolenga kupokea na kutatua kero za wakazi wa kata ya Tinde kwa
kuwahakikishia wakazi hao kuwa tayari EWURA imeidhinisha kushusha bei ya maji katika
kata hiyo. Mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Tinde, kata ya Tinde.
“…. wiki iliyoisha SHUWASA wamenifuata ofisini wakiwa wamepokea barua ya agizo la
kushusha hizo bei kwa mujibu wa sheria kinachofuata ni hatua ya kutangaza kwenye
gazeti la Serikali …..”amesema Wakili Mtatiro
Akitoa salamu za Kata, Diwani wa kata ya Tinde, Mhe. Jafary Makwaya amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea
kata hiyo fedha ambazo zimefanikisha miradi mbalimbali ikiwemo ukarabati wa Shule ya Msingi
Tinde A na B, ujenzi wa bweni na matundu ya vyoo katika shule ya wasichana Tinde na sekondari
Kituri, ujenzi wa barabara ya kutoka Tinde kwenda shabuluba, fedha za umeme wa REA kwa kila
kijiji, ujenzi wa Zahanati ya Ngokoro na mradi wa maji katika kijiji cha Buchama.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Bw. Stewart Makali
akijibu hoja ya wananchi kuhusu ujenzi wa stendi ya Tinde, amesema kuwa tayari Serikali imetoa
kiasi cha shilingi milioni 30 kati ya 50 zilizotengwa na ujenzi wa stendi hiyo utaanza mara moja.
Diwani wa kata ya Tinde, Mhe. Jafary Makwaya akitoa salamu za Kata wakati wa mkutano wa hadhara
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.