Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeziagiza Halmashauri ambazo bado hazijakamilisha ujenzi wa Maabara za masomo ya Sayansi "fizikia, kemia na Baiolojia" kuendelea na ukamilishaji huo. Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru eneo la Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga tarehe 25.08.2018.
"Lakini pia Serikali imeagiza, ndugu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, katika halmashauri yako ya Wilaya kama bado kuna sekondari ambazo hazijakamilisha ujenzi wa maabara tatu, maabara ya Fizikia, Kemia pamoja na Baiolojia endeleeni na ujenzi wa maabara hizi, lengo la serikali vijana wote wanaosoma masomo ya sayansi waweze kusoma masomo haya kwa njia ya vitendo" Amesema Ndg. Kabeho.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.