Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Albert Msovela leo tarehe 05.05.2021 ameitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Kuzungumza na Uongozi. Wakuu wa Idara na Wafanyakazi na kusisitiza sana kuhusu mahusiano baina ya mfanyakazi na Mfanyakazi na Idara na Idara.
Akizungumza kwenye Kikao cha Majumuisho, wakiwepo wakuu wa Idara, Mkurugenzi na Wafanya kazi wote, Katibu Tawala huyo alianza kwa kusisitiza sana Upendo baina ya wafanya kazi na kuwataka wawe kitu kimoja. Alisema "Hata kauli mbiu ya Chama cha wafanyakazi inasema "Solidarity Forever"......ni wajibu na lazima wafanyakazi wa Shinyanga Dc Mpendane na kushirikiana. kuwe na "Coordination" kama ilivo mfumo wa mwili wa Binaadam.
Baadhi ya wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala huyo alisisitiza sana kwa wafanyakazi na Uongozi kuzingatia sana Sheria, kanuni, Maadili na Miongozo mbali mbali ya Utumishi wa Umma kwenye Utendaji wa Kazi zao na Maisha yao kwa ujumla.. alihimiza sana wafanyakazi waishi maisha yanayofanana na utumishi wa Umma. Aliwakumbusha Idara ya Utawala kuwa wao wana jukumu kubwa la kuhakikisha wafanyakazi wanazingatia sana sheria kanuni na taratibu za utumishi wa Umma. " nyie ndio Engine(Utawala) na Maafisa Rasilimali watu). zungumzeni na watu mjuwe shida zao, wakumbusheni wajibu na kuzingatia miongozo ya ufanyaji kazi serikalini mara kwa mara kabla ya kuwachukulia watu hatuwa za kinidhamu. ni vizuri tuelewane na kuwa wakali baada ya kuzungumza na kuridhika kuwa watu wamepewa nafasi ya kubadilika ila hawaoneshi dalili.
Katibu Tawala huyo alisisitiza sana Wafanyakazi kuwa na Siri za kiofisi na kutoku 'share' taarifa au document kwenye njia ambazo sio salama kama vile kutumia whatsapp ama email ambazo sio za Serikali. amewaambia wafanyakazi iwe marufuku uvujaji na usambazi wa kumbukumbu za kiofisi kwa watu wasihusika na shughuli za kiofisi.. aliwaonya wafanyakzi kuwa hatakuwa na simile kwa Mfanyakazi yeyote atevujisha taarifa na kumbukumbu za kiofisi kwani hilo ni miongoni mwa makosa makubwa ya kiutendaji.
Mheshimiwa Katibu Tawala huyo alisisitiza kwa kuzitaka Mamlaka kuwapatia mafunzo kazini wafanyakazi. "Tuwe na Mpango wa Mafunzo kwa wafanyakazi na kada zote na tuhakikishe kila mwaka kuna wafanyakazi wanaongezewa uwezo kwa kuhudhuria mafunzo ya kada zao". Alisisitiza kuona Mpango wa Mafunzo uliofanyiwa 'need Assesment' ya kutosha ili mafunzo hayo yawe na tija kwa wafanyakazi na Halmashauri kwa Ujumla.
Aliwaomya Wafanyakazi kutotegemea wanasiasa na kuacha taaluma zao na miongozo mbali mbali kwa kutaka urahisi kwenye maisha ya kazini hapa Shinyanga DC. "kuna watu wanapenda 'Vitonga, Senkeke'... Miteremko. wanaona wakijuhisisha na wanasiasa basi watakuwa salama kwenye mabaraza ya nidhamu. kawaonya wafanyakazi kuachana na mambo ya kupenda "Miteremko" bali wazingatie sheria, kanuni, maadili na miongozo ya utumishi wa Umma hapo watakuwa salama.
Ugeni wa Katibu tawala huyo uliwahiiza Idara ya utawala na rasilimali watu kuwa na mfumo wa ukusanyaji wa malalamiko ya wafanyakazi na kuyafanyia kazi ili kusiwe na migogoro maeneno ya kazi na kama ikiwepo isiwe ya kutishia maisha ya wafanyakazi na ufanyaji kazi. " Muwe na utaratiu wa wazi na utaozingatia faragha za watu, mpokee 'complains' na mzifanyie kazi hii itaisaidia sana kupunguza migogoro kazini,
kwa Upande wao wafanyakazi, walitaja kero zao na Kumuomba kuwa hiki alichokifanya leo basi kiwe endlevu. walimshukuru sana Katibu tawala kuja kuonana na kusikia kero za wafanyakazi. kitu ambacho kimeondowa woga walokuwa nao juu ya Kiongozi huyo na kwamba leo wamejisikia uhuru fulani kuzungumza nae na wamefarijika sana kushare "Issues zao" na kusikilizana walichokuwa nacho wafanya kazi kama kero. alichukuwa baadhi ya kero kwenda kuzifanyia kazi na zile ambazo aliziweza hapo hapo alizotolea Ufafanuzi.
Akizungumza kwenye kikao hiko, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Bi. Hoja N, Mahiba, (Picha chini)
alisisitiza Wafanyakazi kupendana na kuwa na "Team Work". kama alivotushauri Kiongozi wetu Katibu Tawala, Tupendane, Tushirikiane na kufanye kazi kama Mwili mmoja. alimshukuru sana Katibu tawala kuja na kuzungumza na wafanyakazi, alisema kafurahi sana kusikia wafanyakazi wameelewa sana Ujumbe ulioletwa na Kiongozi huyo toka Mkoani. Mkurugenzi alimkaribisha tena Katibu tawala huyo kila mara atapoona inafaa na anataka kuzungumza na wafanyakazi, Aliamuahidi kusimamia Maagizo yote aliyoyatowa kwenye kikao hiko na kuwa watajitahidi kuzingatia kanuni, sheria, madili na taratibu mbali mbali za utumishi wa umma kuhakikisha kero na maslahi ya Wafanyakazi wa Shinyanga DC yanatatuliwa.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.