Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Magena, amezindua rasmi programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi, na Mendeleo ya Mtoto (PJT-MMMAM). Uzinduzi huo umefanyika Februari 08, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Elimu na Maji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Iselamagazi, Mhe. Isack Sengerema na wadau wengine.
Lengo la programu hii ni kutoa huduma jumuishi kwa watoto katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na afya, lishe, fursa za uwekezaji wa awali, malezi ya mwitikio pamoja na ulinzi na usalama kwa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi nane.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Ndg. Mabuba alisema Programu hii ni juhudi muhimu za kuimarisha huduma za kijamii kwa watoto kuanzia umri wa miaka sifuri hadi nane. Programu hiyo pia inalenga kuhakikisha kuwa watoto wanapata fursa bora za makuzi na malezi, pamoja na ulinzi dhidi ya hatari zozote zinazoweza kuwakabili. Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha ustawi na maendeleo bora ya watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Aidha, Ndg. Mabuba amesisitiza kuwa ulinzi na usalama wa mtoto ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha wanafichua na kulipoti matukio ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili hatua kali ziweze chukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya vitendo hivyo.
Awali, akiwasilisha mada, Mratibu Afya, Uzazi na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Bi. Halima Hamis amesema lengo kuu la uanzishaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM) ni kuwa na uwekezaji unaoratibiwa kwenye maeneo matano ya mfumo wa malezi jumuishi ambayo ni Afya Bora, Lishe, Malezi yenye Mwitikio, Fursa za Ujifunzaji wa Awali na Ulinzi na Usalama. Uwekezaji katika huduma za MMMAM huwasaidia Watoto kufikia upeo wa ukuaji timilifu lakini pia unaleta faida kiuchumi.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Lyidia Kwesigabo alieleza kuwa programu hiyo inahusisha watoto wa umri kuanzia 0-8 kwa sababu umri huo ndio kipindi ukuaji na ujifunzaji huchukua nafasi kwa kiasi kikubwa kiakili, kimwili, kijamii na kihisia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena
Mabuba akizindua programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na
Mendeleo ya Mtoto.
Mratibu wa Afya, Uzazi na Mtoto wa Mkoa wa Shinyanga, Bi Halima Hamis
akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Lyidia Kwesigabo
akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada wakati wa uzinduzi
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba (katikatika) na wadau kutoka Mashirika
na Taasisi zinazojihusisha na masuala ya afya, lishe , ulinzi na usalama
wa mtoto
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.