Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella amewataka wajumbe wa Mabaraza ya Umoja wa Wanawake UWT, Umoja wa Vijana UVCCM na Jumuiya ya Wazazi kuwa karibu na mabalozi wa shina kwani hao ndio mizizi ya chama.
Ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Shinyanga kata ya Didia ambako amekutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Wajumbe wa Mabaraza yote UWT, UVCCM, Mabalozi pamoja na Wazee maarufu wa CCM
Akitoa salamu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Dk Samia Suluhu Hassan amesema anawashukuru sana wananchi wa jimbo la Solwa kwa kuwa jimbo la pili kwa wingi wa kura kwa uchaguzi wa mwaka 2020 na kuwataka kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zijazo.
Aidha amewakumbusha wajumbe kuendelea kuziishi 4R zinazolenga kuleta maridhiano akisema sote ni watanzania na tunadhamana ya kuifanya nchi yetu iwe salama “utofauti wetu kihisia kifikra usitutenganishe katika jamii zetu, lengo letu ni kuleta maendeleo ambayo si ya wana CCM pekee”
Amesisitiza kuwa viongozi na wanachama kwa ujumla kuendelea kuhamasisha watu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja kuhakikisha wanapiga kura kwani ni haki yao kikatiba
Kwa upande wake Mkuu wa Wiliya ya Shinyanga, Mhe. Wakili Julius Mtatiro amesema ameletwa Wilaya ya Shinyanga na Mheshimiwa Raisi ili kutatua changamoto za wananchi hivyo kama kuna mwananchi anadhurumiwa haki zake asisite kumpigia namba 0739420421 na kwamba namba hizo zinatakiwa ziwepo kila Shule Zahanati na Mahakamani,
Vilevile Mbunge wa Jimbo la Solwa Mh. Ahmed Ally ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo akitolea mfano ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambayo imesheheni vifaa tiba vya kisasa na kwamba imesaidia wananchi kutosafiri kwenda kutafuta huduma za afya mikoa mingine.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.