Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Ngassa Mboje amewaagiza Watendaji wa Vijiji kuwasomea Wananchi taarifa ya mapato na matumizi ya fedha zinazopokelewa ili wananchi hao waweze kufahamu fedha hizo zinavyotumika. Ametoa agizo hilo limetolewa wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024. Mkutano huo umefanyika leo Mei 08,2024 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri uliopo makao makuu ya halmashauri Kata ya Iselamagazi.
Akiwasilisha salamu zilizotolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI wakati wa kikao cha ALAT, Mhe. Mboje amesisitiza uwepo wa ushirikiano baina ya Madiwani na Wataalamu wa Halmasahuri ili kuepusha migongano kwa kuwa wote wanajenga nyumba moja
Aidha, amewataka Madiwani na Mtendaji wa Kata husika kuwa na ushirikiano katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato pamoja na uandaaji wa taarifa ili kuepusha mkanganyiko wa taarifa na migogoro kwenye kata.
Naye ,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mwl. Stewart Makali amewataka Watendaji hao kuanza kutekeleza maagizo yaliotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri haraka na kuahidi kusimamia utekelezaji wa magizo hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la
Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya Kata
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Stewart Makali akichangia mada wakati wa
Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Mwakitolyo Mhe. Masalu Lusana Nyese akiwasilisha
taarifa ya maendeleo ya Kata
Diwani Kata ya Itwangi Mhe. Sonya J. Mhela akiwasilisha taarifa ya
maendeleo ya Kata
,
Mheshimiwa Diwani akichangia Mada wakati wa majadiliano ya taarifa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Wataalamu wa Halmashauri wa
Wilaya ya Shinyanga wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa taarifa
za maendeleo ya Kata.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.