MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA MIRADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA
Na. Afisa Habari Shinyanga DC
Mwenge wa Uhuru 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga umekimbizwa kwa kilomita 94.22 na jumla ya miradi 9 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.346 imezinduliwa, imekaguliwa na kuwekewa Jiwe la Msingi.
Mwenge wa Uhuru 2023 ukiongozwa na Ndg. Abdalla Shaib Kaim umeridhishwa na utekelezaji wa miradi yote katika Halmashauli ya Wilaya ya Shinyanga.
Akiongea na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika Uwanja wa Shule ya Msingi Didia, Ndg. Abdalla Shaib Kaim ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa miradi mizuri yenye ubora na kuzingatia viwango na kusisitiza kuhakikisha kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yanafanyiwa kazi.
Aidha Ndg. Abdalla Shaib Kaim ameendelea kueleza kuwa miradi yote ya maendeleo iliopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni miongoni mwa kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi ya dhati kwa Wanashinyanga. Hivyo ahimiza kuendelea kuwa na Umoja na Mshikamano na kumuunga mkono Mhe. Rais kwa mazuri anayoyafanya.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na Mradi wa Tenki la Maji Ishinabulandi, Mradi wa ujenzi wa Vyumba vinne vya Madarasa Shule ya Sekondari Kituli, Mradi wa Vijana Wabunifu Usanda, Mradi wa Hifadhi na utunzaji Mazingira, Mradi wa Kiwanda cha kukoboa na kuongeza thamani ya Mpunga, Mradi wa Gari la wagonjwa na Mradi wa ugawaji Vyandarua.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameshukuru ujio wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Shinyanga ambao umekuja kumulika na kuanganza mazuri yanayofanywa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.