Shule ya Sekondari Zunzuli iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kata ya Mwenge, Kijiji cha Zunzuli. Lengo la mradi huu ni kutoa huduma mbalimbali kama kutumika kwa ajili ya chakula, mahali pa kuendeshea semina na mikutano mbalimbali, kufanyia mitihani ya ndani na nje, kutumika kama ukumbi kwa ajili ya sherehe mbalimbali na shughuli zingine tofauti. Hii imetokana na mikakati ya awamu ya tano inayolenga kuboresha miundo mbinu ya elimu kwa kuenzi na kuzingatia kaulimbiu ya Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere 1964 ya “Elimu ni ufunguo wa Maisha.”
Gharama zilizotumika kukamilisha mradi huu ni Sh.107,833,620.00 ambapo Sh. 97,868,620.00 zimetoka Serikali Kuu, Sh.9,365,000.00 zimetoka Halmashauri na Sh. 600,000.00 mchango wa Wananchi.
Mradi huu ulianza tarehe 01.06.2018 na ulikamilika tarehe 15.10.2018 na kukabidhiwa rasmi tarehe 05.02.2019 chini ya usimamizi wa Bodi ya Shule na Kamati ya Ujenzi kwa mfumo wa Force Account. Pamoja na kukamilika kwa mradi huu, tunaiomba Serikali yetu itusaidie upatikanaji wa nishati ya umeme wa TANESCO kupitia mradi wa REA awamu ya tatu utufikie kwa haraka ili ituweze kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa lengo la kuboresha na kuinua zaidi kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.