Mwenge wa Uhuru umekagua Mradi wa Uhifadhi wa mazingira Shule ya Awali na Msingi Ng’wang’osha wenye thamani shilingi 3,800,000, ambapo kiasi cha fedha shilingi 800,000 kimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na kiasi cha shilingi 3,000,000 imetolewa na Wahisani
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava aliwapongeza Walimu, Wanafunzi na Wadau wengine wa Mazingira kwa utekelezaji mzuri wa mradi huo.
“ Tumeona jitihada nzuri ambazo zinafanyika na Shule ya Awali na Msingi Ng’wang’osha katika uhifadhi mazingira na niseme ukweli wanafanya kazi nzuri” alisema Ndg. Mnzava.
Naye Mjumbe wa klabu ya Mazingira Shule ya Msingi Ng’wang’osha Flora Masuluzu wakati akisoma taarifa ya mradi alitaja faida zitokanazo na mradi ambazo ni kutunza na kuhifadhi uoto wa asili eneo la msitu wa Shule, kuwajengea uwezo Wanafunzi wa kushiriki shughuli za upandaji miti na kutoa Elimu kwa jamii juu ya uhifadhi mazingira.
Aidha, katika mradi huo klabu ya Mazingira imefanikiwa kuwa na vitalu vya miti sita ambavyo ni kama ifwatavyo Kitalu cha Dkt Samia Suluhu Hassan kina miti 712, Kitalu cha Mwl. Julius Kambarage Nyerere kina miti 1479, kitalu cha Mhe. Philip Isdor Mpango kina miti 482, kitalu cha Dkt. Ally Hassan Mwinyi kina miti 394, Kitalu cha Mhe. Anamringi Macha kina miti 291na Kitalu cha Mhe. Julius Mtatiro chenye miti 263.
Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.