MHE. MKUU WA WILAYA MTATIRO AMESIKILIZANA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Mkuu wa Wilaya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro amesikiliza na kutatua kero za wananchi katika mkutano wa wa hadhara uliofanyika 25/03/2024 kata ya Iselamagazi.
Ikiwa ni mkutano wa kwanza wilayani Shinyanga tangu Mhe. Mtatiro ahamishwe kuwa mkuu wa wilaya ya shinyanga. Ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini katika kutumikia wananchi.
Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Mtatiro alisema kazi aliyotumwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuungana na watumishi kutumikia wananchi na moja ya utumishi kwa wananchi ni mawasiliano na ushirikishwaji hasa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha, katika mkutano huo Mhe. Mtatiro alisema Wananchi wawe huru kuwasiliana naye kama kuna ushauri, maoni au changamoto. Alitoa namba yake ya simu ya mkononi kwa Wananchi na kuwasisitiza wawasiliane naye kwa ajili ya utatatuzi wa changamoto.
Hata hivyo Mhe. Mtatiro alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuweka namba yake katika kila Ofisi au Taasisi za Serikali kama vile Shule, Hospitali na Ofisi za Kata ili wananchi waweze kumpata kwa urahisi wakiwa na changamoto na wasisubiri mikutano ya hadhara ili kuwasilisha changamoto zao.
Wakati wa mkutano huo wananchi walipewa nafasi ya kuwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Wilaya. Moja ya Kero zilizotolewa na wananchi ni kutokuwa na umeme Shule ya Sekondari Iselamagazi. Mhe. Mtatiro alimuagiza Meneja wa Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa kupeleka umeme shuleni hapo ndani ya juma moja baada ya malipo.
Naye Diwani wa Kata ya Iselamagazi Mhe. Isack Sengerema alimshukuru mkuu wa Wilaya kufika Iselamagazi kusikiliza na kutatua kero za Wananchi na kumuahidi ushirikiano wakati wa kusimamia miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba alisema Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni kumi (10,000,000) kwa ajili ya kumalizia jengo la kituo cha Polisi Iselamagazi lililojengwa kwa nguvu za Wananchi.
Hata hivyo, Ndg. Mabuba alisema Wananchi wasisite kuwasiliana naye au kufika ofisini kwake kwa changamoto yoyote hasa kutolizishwa na huduma za watumishi katika ofisi za serikali.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.