Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Kalekwa Kasanga amekutana na Wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wananchi. Ametoa maelekezo muhimu kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo Septemba 26, 2014.
Msimamizi wa Uchaguzi amewataka wananchi wote wa Halmashauri Wilaya ya Shinyanga kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wenye sifa kujitokeza kwa Wingi kujiandikisha tarehe 11/10/2024 hadi 20/10/2024 na kupiga kura tare 27/11/2024 kwa Mujibu wa kanuni 13 (GN571) ya kanuni ya ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa wa Halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya.
Hata hivyo , amezitaja sifa za mkazi atakayekuwa na haki ya kupiga kura ambazo ni pamoja na Awe raia wa Tanzania, awe na Umri wa miaka kumi na nane au zaidi, awe mkazi wa eneo la kitongoji, awe na akili timamu na awe amejiandikisha kupiga kura katika kitongoji husika.
Dkt. Kasanga alisisitiza na kuwasihi wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kufanya Uchaguzi kwa Amani na utulivu bila kuvuruga Amani ya Nchi.
" Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.