Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt Kalekwa Kasangwa ameapishwa kuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Uapisho huo ulioenda sambamba na kula kiapo cha uaminifu na kutunza Siri, umefanyika Leo Septemba 15,2024 katika Ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Shinyanga mbele ya Kamishina wa viapo wa serikali Wakili Mboneke Ndimubenya.
Mapema kabla ya kiapo Wakili Ndimubenya alielekeza juu ya Umuhimu wa viapo hivyo na kusisitiza Utii wa Sheria na kwenda kutenda haki wakati wote wa uchaguzi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024 huku kauli mbiu ya ikisema "Serikali za Mitaa,Sauti za Wananchi,Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.
MSIMAMIZI WA UCHAGUGUZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA AKILA
KIAPO MBELE YA KAMISHNA WA VIAPO WAKILI MBONEKE NDIMUBENYA.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.