Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amefungua vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Solwa B wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi huo Agosti 12, 2024.
Akisoma taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Neema Salim Masawe amesema kuwa ujenzi wa mradi huo umekamilika na utasaidia kuongeza miundbinu ya madarasa katika shule hiyo kwa kuwa itaweka mazingira wezeshi ya kupokea wanafunzi hasa wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2025. Mradi huo umegharimu kiasi cha shlingi 78,000,000.
Aidha, Masawe amewasilisha salamu za shukrani kwa Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua mahitaji ya wananchi wa Solwa na kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia miundombinu ya elimu.
Akipokea salamu hizo za shukrani kwa niaba ya Rais, Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amesema Dr. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha za miradi ya elimu nchini ili wanafunzi wapate mazingira wezeshi ya kujifunzia.
Shule ya Sekondari Solwa B ipo katika Kata ya Solwa ilisajiriwa na kuanzishwa Januari 11, 2023 ikiwa na jumla ya wanafunzi 276 (wasichana 147 na wavulana 129) na walimu watano. Kwa sasa shule hii ina jumla ya wanafunzi 375 (wavulana 135, wasichana 240) na walimu 13 ambapo walimu 10 ni wanaume na watatu ni wanawake
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.