Na. Dhulkifl H. Sungura - Kaimu Afisa Habari
MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA MHE. JOHARI SAMIZI LEO TAREHE 02 FEBRUARI 2023 AMEZUNGUMZA NA WATENDAJI WA KATA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA. AKIZUNGUMZA NA WATENDAJI HAO KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI HIYO, MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA ISELAMAGAZI.
“Mimi na Kamati ya Ulinzi na Usalama tunajipanga kuanza kukaguwa Miradi ya Maendeleo Shinyanga DC sasa kabla hatujaanza ZIara zetu, Watendai hakikisheni mnaweka taarifa zote sawa, za Miradi ya Maendeleo ili njia yetu wakati wa Ukaguzi iwe rahisi”. Lakini kingine alichosisitiza ni kuhakikisha Miradi yote ya Maendeleo kama ilivopangwa na kutekelezwa na Serikali ni lazima tuhakikishe inatimia na malengo yake kufikia. Tumepewa Dhamana na Mhe. Rais, hii ni heshima kubwa, lazima wote tuhakikishe hatumuangushi Mhe Rais wetu Mpendwa, hivyo Miradi ikamilike kwa kiwango ili hata Serikali ikija kuona miradi yake ijuwe kuwa kuna watu waliisimamia vyema.
Akizungumza kwenye Kikao kazi hicho, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KU) ya Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dr. Nice R. Munissy na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje alisema kuwa ni lazima Jamii ijitahidi kuhakikisha inatafsiri MAONO ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo, hivo Wanafunzi wote wenye Sifa za kwenda Shule hawana budi kwenda Shule. “ Mh. Rais Kajenga Madarasa, Kaweka Madawati, anataka Watoto wote waende shule, sasa nasikia tuna Asilimia kama 11 na 10 kwa Msingi na Sekondari kuwa hawajaripoti shuleni,sitakubali nataka Asilimia 100 wote waende shule” Alisisitiza Mhe. Mkuu wa Wilaya. Asisitiza kuwa hata kama Mtoto hana sare za shule au Viatu, ni Agizo la Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwa waripoti shuleni hivo hivo,ili lengo litimie. Asisistiza Michenye itumike kweye Shughuli za Maendeleo pia na si kutumika tu mara watu wanapofumaniwa na wake za wat utu!!!
Akiongelea kuhusu Mazingira, Mheshimiwa DC Samizi alisema ameridhishwa alivokuwa njiani kutokea Manispaa ya Shinyanga alipoanza kuingia tu OLD SHINYANGA aliona kidogo kuna dalili za Uhai na kamwe sio kama huko alikotokea kwani kidogo kulikuwa na ukame sana. “ hapa nimeona dalili ya Uhai, hakuna misitu mingi, lakini kwa kweli kuna Dalili kabisa ya uhai, hili limenifurahisha. Kwani mimi nimuumini mkubwa wa Masuala ya Kutunza Mazingira, na ni lazima tuhimizane kuhakikisha Mazingira yetu yanakuwa safi na Salama na Miti haikatwi katwi hovyo”. Alisisitiza kuwa Mazingira usipoyatunza basi ujiandae na yenyewe kukuadhibu,ukiyadharau na yenyewe yatakudharau, sitaki kuona swala la mazingira Shinyanga DC yanadharauliwa.
Asisitiza ni kutekeleza takwa la kisheria kusoma mapato na matumizi kwa wananchi. Wanancho wana haki ya kujuwa mapato na matumizi ya Nguvu zao zote wanazojitolea kwenye Miradi ya Maendeleo na kamwe sio kuwaomba tu michango bila kuwapa taarifa za Mapato yao na matumizi yao. Asema Vijijini ni tatizo sana kusikia kwenye Mikutano mikuu ya vijiji Ajenda hiyo ikisomwa.
DC Samizi alisisitiza ili kuhakikisha Malengo ya Wilaya yanatimizwa, ni lazima wote tushirikiane, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wote, Bila ushirikiano wenu mimi Mkuu wa Wilaya nakuwa si lolote si chochote, nawaomba sana Tushirikiane kuhakikisha Gurudmu la Maendeleo kwenye Wilaya yetu linasonga mbele.
Akimaliza kikao kazi Hicho, Mhe, Mkuu wa Wilaya aliongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwenda Kwenye Baraza la Madiwani kupitia, kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 23/24.
Aliwapongeza Halmashauri kwa Bajeti nzuri na Waheshimiwa Madiwani jinsi walivoijadili na kuhimiza Vipaumbele vyote vilivoibuliwa na Waheshimiwa Madiwani havina budi kutekelezwa kwenye Bajeti ya mwaka 23/24. "Bajeti ni nzuri, mjipange kuhakikisha Vyanzo vyote vya Mapato mlivovikasimia mnavikusanya na kuwa Mtatumia kadiri mlivojipangia".
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.