Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh. Jasinta Mboneko na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Hoja N Mahiba waongoza Zoezi la Upandaji Miti Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ki Halmashauri yalofanyika katika Kijiji cha Ihalo, Kata ya Ilola leo tarehe 27/11/2020
wakiwa na Afisa Misitu wa Halmashauri, Bi. Juliana Mollel. Mkurugenzi alimueleza Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kuwa Hadi kufikia Novemba 2020 Miche ya Miti 18,500 imesambazwa na inaendelea kupadwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya. Miche 5,000 imepandwa kwa Juhudi za Taasisi zisizo za Kiserikali na watu binafsi na Miche 13,500 inaendelea kuandwa katika maeneo ya Taasisi za umma zikiwemo Shule, Vituo vya Afya na Ofisi za Vijiji na Kata.
Akiwashukuru Wadau, Bi Hoja alisema " Kwa Namna ya Pekee napenda kutowa shukrani zangu za dhati kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Williamson Diamond (Mwadui) kwa kujitolea na kuipatia Halmashauri miche ya miti 18,500".
MkurugenziMTendaji Bi. Hoja N Mahiba, Alimshukuru sana Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Ofisi yake na Mkoa kwa Ujumla kwa Maelekezo na ufuatiliaji wao Katika kuwezesha Shinyanga ya Kijani, Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza kuwa MITI NI UHAI
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.