MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alifanya Ziara Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kata ya Mwalukwa 26/09/2023.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme aliweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Tanki la Maji lenye ujazo wa Lita 100,000 pamoja na bomba kuu la maji lililojengwa kwa ushirikiano wa Life Water International pamoja na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Mradai huo unaoetekelezwa katika Kijiji cha Bulambila Kata ya Mwalukwa una jumla ya mtandao wa Kilometa Thelathini na Nne (KM 34).
Inakadiliwa Mradi huo utahudumia Wananchi zaidi ya Elfu nane na mia nne (8,400) kwa maji safi na Salama katika Vijiji vinne (4) vya Mwalukwa, Bulambila, Kadoto na Ng'hama. Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Mhe. Mndeme alisema, Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina uhusiano mzuri sana na Mashirka yasiyo ya Kiserikali na ndiyo sababu leo tunashuhudia kukamilishwa utekelezaji wa Mradi huu muhimu ambao umekuja kuondoa kero hapa Kata ya Mwalukwa huku akiwataka Life Water International na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA )kuona namna ya kuongeza Tanki na mtandao wa Maji zaidi ili uweze kuwahudumia Watu wegi zaidi.
Mhe. Mndeme pia alikaguwa na kutembelea ukarabati wa Bwawa la Maji Mwalukwa ambalo awali lilikuwa na kina cha Mita 2.25 na sasa litakuwa na kina cha Mita 4.1 ambapo kwa upande wa ujazo wa lita za Maji awali lilikuwa ni zaidi ya lita elfu 71 na litakapokamilika litakuwa na ujazo wa lita zaidi ya laki 2.93.
Ukarabati huu wa Bwawa unakwenda kuwanufaisha wananchi zaidi ya elfu 22 ambao watawekea Birika kwa ajili ya kutumia maji haya na mifugo zaidi ya 13 ambapo kutaondoa kabisa kero ya uhaba wa maji eneo hili.
Mkuu wa mkoa amekili kufurahishwa na utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa ya maji amabayo itatua kero ya upungufu wa maji Kata ya Mwalukwa.
Aidha, amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini na Wananchi wa Kata ya Mwalukwa katika utekelewaji wa miradi hiyo.
Amewapongeza wananchi wa mwalukwa kwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi hiyo . alisema “ Nawapongeza sana Wananchi wa Kata ya Mwalukwa kwa kushiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa bomba na kutoa maeneo yenu ili kuwezesha miundimbinu ya mradi ijengwe.
Mhe. Mndeme ilihitimisha Ziara hiyo kwa kufanya Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwalukwa ambapo alisikiliza na kutatua Kero za Wananchi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.