Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mdeme amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri za Wilaya ya Shinyanga, Kishapu na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa vipaumbele vya bajeti za halmashauri vinazingatia msingi unaoleta tija kwa maslahi ya wananchi. Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa kikao kazi kilicholenga kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Mhe. Mdeme amezielekeza halmashauri hizo kutafuta namna bora ya ukusanyaji mapato na kuziba mianya yote inayopelekea upotevu wa mapato ya Serikali, kuweka mikakati itakayowezesha kukamilisha miradi ya mendeleo kwa wakati na kushauri kuwa mikakati hiyo iwekewe mpango kazi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Kisena Mabuba amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa halmashauri imejipanga kwa kuweka mikakati madhubuti ambayo itasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Baadhi ya mikakati hiyo inatekelezwa na imeanza kuzaa matunda. Mikakati aliyoitaja ni pamoja na kufuatilia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na wa kushtukiza ili kuziba mianya ya wizi, kutoa elimu kwa wafanyabiashara, kuandaa kanzi data ya wafanyabiashara wote, kuwezesha wakusanya mapato kwa kuwapatia vitendeea kazi muhimu na kuongeza mashine za kukusanya mapato.
Akizungumzia vipaumbele vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Bw. Mabuba ameainisha kuwa halmashauri imejipanga kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuimarisha utawala bora na uwajibikaji, kuboresha upatikanaji wa huduma zenye ubora za jamii katika sekta mbalimbali, kukarabati na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya huduma za kijamii, na kumalizia ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Mkude amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri ya Wilaya za Sinyanga, Kishapu na Manispaa ya Shinyanga kutekeleza shughuli za maendeleo kwa ukamilifu wake na kutenga fedha kwa ajili ya vipaumbele vya wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Shinganya imependekeza bajeti ya Tsh. Billioni 40.5 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa shughuli za halmasahuri na miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mdeme akizungumza na
Wakurugenzi pamoja na wataalamu kutoka halmashauri za wilaya ya
Shinyanga, Kishapu na Manispaa ya Shinyanga wakati wa kikao kazi
Februari 12, 2023
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Bw. Kisena Mabuba
akifafanua jambo wakati wa kikao kazi
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu , Mhe. Joseph Mkude akizungumza wakati
wa kikao
Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakifuatilia
kwa karibu wakati wa kikao.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.