Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme Tarehe 6 Disemba, 2023 amewatembelea wahanga wa maafa walioezuliwa na kubomolewa makazi yao katika kata ya Mwamala kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia terehe 6 Disemba, 2023.
Akizungumza na Wahanga hao Mhe. Mndeme amewapa pole na kuwaeleza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imepokea maa masikitiko makubwa taatifa za mafuriko haya na kwamba sasa serikali itatoa huduma ya matibabu bure mpaka kupona kwa Majeruhi wote, italeta mbegu kwa Wathirika wa Mashamba, italeta Vifaa vya kulalia na itafanya tathimini ya awali ili kujuwa kiasi cha hasara iliyopatikana na mahitaji halisi.
"Poleni sana Ndugu zetu kwa tukio hili, lakini tu niseme kuwa serikali itagharamia matibabu wa Majeruhi, kuleta Mbegu, vifaa vya kulalia, pia nimuagize Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kufanya tathimini ya awali kujuwa uhalisia wa mahitaji na hasara iliyopatikana ili Serikali ijue, niseme tu kuwa, haya ndiyo maelekezo ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wahanga wote," alisema Mhe. Mndeme.
Aidha ,Kata ya Mwamala jumla ya nyumba 51 zimeathirika na mvua hizo pqmoja na hekari takribani 10 kuharibiwa kabisa na mvua ya barafu iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Ng'onze sanjali na kuumiza watu wanne akiwemo bibi kizee ambaye amelazwa hospitali ya Mwawaza.
Mhe. Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ya mvua hizi zilizotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa zitakuwa za juu ya kiwango, kuondoka maeneo yote hatarishi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.