Na Monica Mnanka, Shinyanga DC
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bw. Saidi Kitiga akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo ametoa wito kwa
wote wakataoshiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki za ardhi
unaotarajiwa kuanza Julai mosi 2024 kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu kwa kuzingatia uzalendo.
“ Niwasihi kila mmoja wetu kwa nafasi yake atimize wajibu wake kikamilifu ili kuleta matokeo chanya......., tuunganishe
nguvu zetu kwa pamoja kuwezesha maeneo yetu ya vijiji 15 kupangwa, kupimwa na kusimamiwa vyema kwa ustawi
wa Taifa letu.” Alisisitiza Bw.Kitiga
Hayo ameyasema Juni 28,2024 wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa mradi huo uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga uliopo Iselamagazi. Katika mkutano huo pia
amewataka watekelezaji wa mradi kutekeleza majukumu yako kwa weledi, haki na usawa ili kuepusha migogoro
kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Bw. Kitiga amesema mradi huo umelenga kuboresha usalama wa milki za
ardhi kwa kupanga , kupima na kusajili milki ardhi ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inakusudiwa
kutoa Hati Milki 62,000 katika maeneo ya vijiji 15 vya kata 9 . Vijiji hivyo ni pamoja na kijiji cha Samuye, Isela,
Singita, Jomu, Nyambui, Didia, Mwanono, Solwa, manheigana, Songambele, Mwakitolyo, Nyaligongo, Iselamagazi,
Mwamakaranga na mwongozo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Edward Maduhu akitoa neno la ufunguzi
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan mradi ambao
unakwenda kutatua na kuondoa kero mbalimbali za ardhi ikiwemo kuwapatia hati milki na kuondoa migogoro
ya mipaka.
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni miongoni mwa zaidi ya halmashauri 60 zinazotarajiwa kunufaika na mradi huo.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.