MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA NNE 2022/2023
Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Kata kwa kipindi cha robo ya nne 2022/2023
Mkutano huo Umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, uliopo Makao Makuu ya Halmashauri - Kata ya Iselamagazi, leo Tarehe 10 Agosti 2023, na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje.
Mkutano huo wa kawaida wa Baraza la Madiwani umehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Shinyanga, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Watumishi, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Waandishi wa Habari na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Katika Mkutano huo Waheshimiwa Madiwani waliwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Kata zao, taarifa zote zilipokelewa, zilijadiliwa na kupitishwa.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.