Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Kata kwa kipindi cha robo ya Kwanza 2023/2024
Mkutano huo Umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, uliopo Makao Makuu ya Halmashauri - Kata ya Iselamagazi, leo Tarehe 1 Novemba 2023, na kuongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nicodemus L. Simon.
Mkutano huo wa Baraza la Madiwani umehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Watumishi, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Waandishi wa Habari na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Katika Mkutano huo Waheshimiwa Madiwani wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Kata zao, taarifa zote zilipokelewa, zilijadiliwa na kupitishwa.
Akizungumza katika Mkutano huo wa baraza la Madiwani Makamu mwenyekiti amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hususani Sekta Za Afya na Elimu.
Mhe. Makamu Mwenyekiti amewataka Wataalam wa Halmashauri kutatua changamoto zilizo tajawa kwenye taarifa izo za Kata hasa kuweka mkakati wa kumalizia ujenzi wa Maboma ambayo yamejengwa kwa nguvu za Wananchi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. David Rwazo Amehaidi kutekeleza maagizo yote yaliotolewa katika kikao hicho
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.