Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Bi. Hoja N. Mahiba Atembelea Wachimbaji wa Madini ya Dhahabu Mgodini Nyandolwa, Mwenge, Shinyanga DC leo tarehe 31/07/2021
Bi. Hoja akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Wachapakazi Gold Mine waendeshaji wa sehemu ya Mgodi wa Dhahabu wa Nyandolwa leo tarehe 31/07/2021 alipowatembelea Ofisini kwao.
Akieleza Changamoto zinazowakabili kwenye mgodi huo, bwana Sylvester, Mwenyekiti wa Wachapakazi Gold Mine alisema kumekuwa na Changamoto za mgawanyo wa maeneo ya kufanyia shughuli za uchimbaji lakini wameshazifikisha Serikalini kwa utatuzi,ila alisema hali ya Amani na usalama mgodini ni nzuri sana.
Bi. Hoja alimueleza Mkiti huyo kuwa asiwe na wasiwasi wa Changamoto zake kwani Serikali ya Jamhuri wa Tanzania ni sikivu. Imesikia kero zao na inazishughulikia.
Bi Hoja Aliwapngeza sana Wachapa kazi na alisema “ Kwa kweli kama Jina lenu linavosadifu, nimefurahishwa sana na Juhudi mnazozionyesha kwani kila nikija kuwatembelea hapa nakuta mabadiliko makubwa,ni ishara kuwa mnachapa kazi kweli kweli” Alisema.
Aliwasisitiza kudumisha suala la Amani mgodini, kulipa kodi zote za Serikali na Mrahaba. Na kuwasisitiza kuwa kukiwa na changamoto yeyote basi wasisite kuijulisha Serikali ili iweze kuipatia ufumbuzi kwa haraka. Alisisitiza umuhimu wa kushirikiana kwenye kutatuwa changamoto mara tu zinapojitokeza hapo mgodini
.
Bi Hoja aliendelea na ziara yake kwa kupitia maduara yote ya Uchimbaji na kuongea na baadhi ya wachimbaji na wakaguzi wa Madini Mgodini.
Wachimbaji walimwambia mambo yanaenda vizuri na changamoto za kawaida zinazojitokeza basi viongozi wa migodi na wakaguzi pamoja na Tume ya Madini wanaendelea kuzitatuwa mara tu zinapojitokeza. Bi Hoja Aliwasaidia Baadhi ya Wachimbaji kutowa mfuko wa Udongo wenye dhahabu kama inavoonekana pichani hapa chini.
Bi Hoja Alihitimisha ziara yake kwa kuwaahidi wachimbaji na vingozi wao kuwa sasa atakuwa akiwatemelea mara kwa mara ili ahakikishe changamoto zao walizomueleza anazitatuwa haraka kdiri zitavokuwa zinajitokeza.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.