Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Kalekwa Kasanga amewaomba Wadau wanoatekeleza afua za Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kuendelea kupaza sauti na kutoa elimu ya kutokemeza ukatili ili kunusuru kundi hilo.
Ameyasema hayo akiwa anahairisha kikao cha kamati ya ulinzi wa Wanawake na Watoto ngazi Halmashauri leo Oktoba 23, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo kipeekee ameishukuru taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Tanzania (WFT-TRUST) kwa kuiwezesha Halmashauri takribani miaka 6 kutekeleza shughuli mbalimbali za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Sambamba na hatua zinazoendelea za kubadili umri wa Watoto wa kike kuolewa bado kama wadau endeleeni kupambania hali ya ulinzi na usalama wa Mwanamke na Mtoto” Dkt. Kasanga ameongeza.
Kwa upande wake Mratibu wa MTAKUWWA Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Aisha Omari amesema kupitia utekelezaji wa mpango huo kwa mwaka huu wameweza kuwaokoa Wanafunzi 7 wa kike katika ndoa za utotoni na wawili kati yao kuwarejesha shule za Sekondari za bweni za Salawe na Isaka.
Aidha, Bi. Aisha ameongeza kuwa mbali na mafanikio mengi wamefanikiwa pia kufanya uratibu na uundwaji wa madawati na mabaraza ya watoto nje na ndani ya shule na kufanikiwa kupata madawati 144 ya shule ya Msingi na 32 ya Sekondari. Mabaraza 20 ya Kata pamoja na Mabaraza 99 ya Vijiji yanayoendelea na kazi za kuelimisha maswala ya ukatili nje na ndani ya shule.
Akitoa neno la shukrani kwaniaba ya Wadau wengine Meneja Miradi kutoka shirika la Thubutu Africa Initiative (TAI) Bi. Pascalia Mbuguni amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kupokea changamoto na mapendekezo yao, pamoja na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutoa elimu kwa jamii ili waweze kuachana na mila na desturi kandamizi zinazopelekea kufanya ukatili dhidi Wanawake na Watoto.
Awali wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Ndg. David Rwazo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji aliwakumbusha Wadau mbali na kupigania kundi la wanawake na watoto vile vile wasisahau kuwaelemisha wanaume umuhimu wa elimu jumuishi katika malezi ya familia.
Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ni mpango kazi wa Taifa wa miaka mitano mpango ambao ulipelekea Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Wadau kuandaa mkakati wa Mkoa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kuangalia changamoto za Mkoa na kuziwekea mikakati ya utekelezaji.
Mkakati huu katika Halmashauri ya Wiliya ya Shinyanga umetekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali YAWE, RAFIKI SDO, POLISI DAWATI LA JINSIA NA WATOTO WILAYA YA SHINYANGA ,YWL, GCI, SPC, WEADO, RADIO FARAJA NA Halmashauri ya Shinyanga yenyewe kwa awamu mbalimbali kupitia fedha ya ruzuku kutoka (WFT-TRUST).
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.