MKURUGENZI MTENDAJI AFANYA KIKAO KAZI NA WATENDAJI WA KATA
Na Afisa Habari Shinyanga DC
Maafisa Watendaji wa Kata wametakiwa kufanya kazi kwa kufwata taratibu, kanuni na sheria za Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg; Simon Berege ametoa maagizo hayo katika kikao kazi cha kusikiliza na kutatua changamoto wanazo kutana nazo Watendaji wa Kata katika maeneo yao ya kazi. Pia kuhimiza kuongeza juhudi za ukusanyaji mapato na usimamizi wa Miradi Ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri.
Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi Berege amewataka Maafisa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanafanya vikao na wananchi ili kuongeza uelewa na ufahamu katika Jamii juu ya Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Nakutumia vikao ivyo kama majukwaa ya kutoa Elimu kwa jamii juu ya mfumo wa mapato wa Tausi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ametoa maelekezo yafwatayo;
1. Kutengeneza Mkataba wa makabidhiano wa mashine za POS kati ya Halmashauri na Watendaji wa Kata.
2. Kuimarisha ushirikiano kati Watendaji wa Kata na watumishi wengine wa Halmashauri katika zoezi la ikusanya mapato ili kuongeza mapato ya Halmashauri.
3. Vikao vyote vya kisheria vifanyike kwa wakati.
4. Kufungua ofisi kwa wakati, muda wa kuanza kutoa huduma ni 1:30 Asubuhi.
5. Elimu ya mfumo wa mapato wa TAUSI itolewe kwa Watendaji wa Kata
Mwenyekiti wa Maafisa Watendaji wa Kata akiaongea kwa niaba ya Watendaji wa Kata alisema “ tutasimamia ukusanyaji wa mapato kwa uwadilifu na uwaminifu mkubwa kwa kushirikiana na timu ya usimamizi wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri.
Akifunga kikao Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya shinyanga Mhe; Ngasa Mboje alihimiza Watendaji wa Kata kutimiza wajibu na kufwata taratibu zilizowekwa. Pia kuongeza juhudi za ukusanyaji mapato na usimamizi wa Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata zao.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.