MKOA WA SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUZINDUWA MIRADI MBALI MBALI, SHUGHULI ZA KUTUNZA MAZINGIRA NA MICHEZO MBALI MBALI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA
NA AFisa Habari Shinyanga DC
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Chrisitian Solomon Mndeme tarehe 26/04/2023 ameongoza wakazi wa Mkoa wa Shinyanga katika kuadhimisha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuzindua Miradi mbalimbali Manispaa ya Shinyanga na kuwataka Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha Miradi inatunzwa ili kunufaisha Vizazi na vizazi vijavyo.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya MAsekelo, Mhe. Mndeme aliwaambia wananchi hao kuwa ni muhimu sana kuendelea kujivunia Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa ndiyo umeweza kuwakutanisha leo katika tukio hilo muhimu kabisa la uzinduzi wa Zahanati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Çhama Cha Mapinduzi yam waka 2020 ambacho kilizaliwa kutoka katika Muungano ambao leo una miaka 59.
"Ndugu zangu wananchi, leo tupo hapa kwenye tukio muhimu kabisa tena linalohusu afya za watu wetu tukiwa na amani, upendo, mshikamano na udugu wetu huu mnaouona ni matunda ya Muungano ulioasisiwa na viongozi wetu Sheikh Abeid Amani Karume aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwl Julius Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanganyika wakati huo. Hivyo ni muhimu sana kwetu sisi tunapokwenda kuadhimisha sherehe hizi tuuenzi Muungano wetu, tuwaenzi waasisi wa Muungano kwa kudumisha upendo, amani na mshikamano," alisema Mhe. Mndeme.
Awali akifungua maadhimisho hayo katika viwanja vya Zimamoto aliwahutubia wananchi waliokuwa wamejaa uwanjani hapo alisema Shinyanga inajivunia Muungano kwa kuwa imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbalimbali ikiwamo Elimu, Afya, Miundomniju, ustawi wa wananchi kiuchumi nk.
Alieleza kwa ufasaha hatua zote za maendeleo zilizopigwa katika Nyanja zote tangu uhuru akilinganisha na sasa, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alitaja mafanikio makubwa yaliyoletwa baada ya kuungana na kusema ni lazima wana Shinyanga tujivunie sana mafanikio yaliyopatikana.
Pamoja na mafanikio lukuki yaliyopatikana ndani ya miaka 59 ya Muungano, lakini Mkoa wa Shinyanga umepiga hatua kubwa sana katika Elimu ambapo miaka 59 iliyopita mpaka sasa Shinyanga ina jumla ya shule 646 huku akielezea upande wa Afya kuwa miaka 59 iliyopita Mkoa wa Shinyanga ilikuwa na Zahanati 10 tu, ambapo mpaka kufika leo kuna jumla ya Zahanati 250.
Kwa Upande wa Shinyanga Dc, Maadhimisho hayo yaliitimishwa tarehe 25/04/2023 kwa kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo upande miti, zaidi ya Miche 1,000 ilipandwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga pamoja na shughuli mbalimbali ikiwemo michezo mbali mbali ya Draft, kucheza bao na michezo ya mpira, ambapo timu ya mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ilishindana na timu ya wana zengo toka iselamagazi.
kuona Video tafadhali funguwa kiungo kifuatacho https://www.youtube.com/watch?v=SlShHNHckxU&t=141s
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.