Mwenge wa Uhuru Wilayani Shinyanga umepokelewa tarehe 13.05.2019 katika kata ya Pandagichiza kijiji cha Shilabela ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019 katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ulikimbizwa kwenye urefu wa kilomita 81.4 na ulipitia miradi 9, kati ya hiyo, miradi 2 imezinduliwa, 1 umeonwa, 2 imewekewa jiwe la msingi, 2 imefunguliwa na miradi 2 umekabidhiwa. Miradi yote hii ina thamani ya jumla ya shilingi 812,653,723.00 kwa mchanganuo ufuatao: -
1. Sekta binafsi Sh.......................................... 145,037,430.00
2. Halmashauri Sh ......................................... 34,365,000.00
3. Serikali kuu Sh .......................................... 581,958,593.00
4. Wananchi Sh .............................................. 51,292,700.00
Jumla ........................................................................ 812,653,723.00
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ipo katika Sekta za Elimu, Maji, Afya na Maendeleo ya Jamii. Pamoja na kupitia miradi ya maendeleo, Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2019 zimebeba ujumbe usemao “Maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serekali za Mitaa” Ujumbe huu unaambatana na kauli za uhamasishaji kuhusu:-
Mapambano dhidi ya RUSHWA chini ya kauli mbiu “Kataa Rushwa, Jenga Tanzania”.
Mapambano dhidi ya UKIMWI chini ya Kauli Mbiu “Pima, Jitambue, Ishi”.
Mapambano dhidi ya DAWA ZA KULEVYA; chini ya Kauli Mbiu “Tujenge Maisha Yetu, Jamii Yetu na Uhuru wetu Bila Dawa za Kulevya”.
Mapambano dhidi ya MALARIA chini ya Kauli Mbiu “Nipo Tayari kutokomeza Malaria, Wewe je”.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.