Vijana 18 kutoka Kikundi cha Bodaboda Solwa, Kata ya Solwa wamesema kuwa hali yao ya kiuchumi imeboreshwa kutokana na mkopo wa shilingi 26,000,000 wa mwaka 2021 ikiwa ni mikopo ya kuwawezesha vijana kiuchumi inayotolewa na Halmashauri.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa kikundi hicho cha bodaboda, Ndg.Patrick Victor Katwale wakati akisoma taarifa ya shughuli za kiuchumi za kikundi hicho kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava wakati Mwenge ulipopita kukagua mradi huo Agosti 12, 2024.
Akielezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na mkopo huo, Kitwale amesema hadi sasa vijana sita wamefanikiwa kujenga nyumba za kisasa ambazo wanaishi, vijana wawili wamenunua viwanja, kikundi kimejenga banda ( kijiwe) eneo la senta Solwa ambalo huwakinga na jua pamoja na mvua.
Mafanikio mengine ni pamoja na kufanikiwa kununua pikipiki 11 baada ya kikundi kuongeza fedha na pia kikundi kimepata cheti cha pongezi kutoka halmashauri kwa kumaliza rejesho la mkopo huo kwa wakati.
Naye Mnzava akizungumza na vijana hao, ameipongeza Serikali kupitia halmashauri kwa kuwawezesha vijana kiuchumi na amewaasa vijana nchini kuhakikisha wanafanya marejesho ya mikopo ilitotolewa na Seikali ili kiwezesha vijana wengi zaidi waweze kunufaika na mikopo ya Serikali.
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ilitekeleza programu ya mfuko wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama ilivyo kwa Halmashauri zote nchini kufuatia agizo la Serikali la mwaka 1998 kuwa Halmashauri zote nchini zianzishe mfuko huo kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani.
Kwa sasa halmashauri inaendelea kutenga 10% ya mapato yake kwa ajili ya mikopo kwa makundi tajwa wakati ikisubiri maelekezo ya Seikali kuhusu utaratibu mpya wa program ya utoaji mikopo kwa makundi hayo
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.