Mbunge wa jimbo la Solwa Mh.Ahmed Ally Salum leo tarehe 05 Julai , 2019 amefanya ufunguzi wa shule mpya ya sekondarin ya Mwalukwa iliyopo katika kata ya Mwalukwa wilayani Shinyanga.Shule hiyo yenye jumla ya vyumba vitano vya madarasa ,ofisi moja ya walimu ,maabara mbili ,matundu mawili ya vyoo vya walimu , nyumba mbili za walimu pamoja matundu manne ya vyoo vya wanafunzi.
Kutoka upande wa kulia Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Ally Salum ,kati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Hoja N. Mahiba pamoja na Mhe.diwani na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya,Elimu na Maji kutoka kata ya Masengwa Ndg. Nicodemus L. Simon.
Shule ya sekondari Mwalukwa imesajiriwa kwa namba S.5205 ina jumla ya wanafunzi 214,wasichana 114,wavulana 100.Mpaka sasa ina kidato cha kwanza mpaka tatu. Ujenzi wa shule umekamilika kwa kutumia fedha za Halmashauri ,Mfuko wa jimbo pamoja na nguvu za wananchi.
Kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekondari Mwalukwa kutapelekea mafanikio makubwa ya kielimu ndani ya vijiji vya kadoto,ng'hama,bulambila na mwalukwa vilivyopo katika kata hiyo lakini pia kutapunguza umbali kwa wanafunzi ambapo hapo awali walikuwa wakiladhimika kutembea zaidi ya kilomita kumi ili kufika shule ya sekondari Pandagichiza.
"Kukamilika kwa ujenzi shule hiyo kutasaidia kuboreshwa kwa elimu kwani hapo awali hapakuwa na shule ya sekondari katika kata hiyo,alisema Afisa elimu wilaya ndg.Stewart Makali".
Mhe. Mwenyekiti Bw. Ngassa S. Mboje alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Mwalukwa wakati wa ufunguzi wa shule ya sekondari Mwalukwa iliyopo katika kata ya Mwalukwa Wilayani Shinyanga.
Aidha shule ya sekondari Mwalukwa inakabiliwa na upungufu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo:-
- Upungufu wa maabara ya Chemistry,nyumba nne za walimu,jengo la utawala,vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo,pamoja na viti na meza za wanafunzi.
Mikakati iliyopo kuanzishwa kwa ujenzi mwingine wa vyumba vitano vya madarasa vyenye thamani ya Tshs. 85,075,272/-.
Pia halmashauri kwa kushirikiana na mdau wa maendeleo kutoka shirika la peace coop ina mpango wa kujenga matundu 16 ya vyoo, vyenye gharama ya Tshs. 30,595,413.60/- ambapo jamii iliyopo inatakiwa kuchangia asilimia 25 ambayo ni sawa ni Tshs.7,648,853.4/-.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.