Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum Ally leo tarehe 16.09.2021 akiwa kwenye Ziara ya Madiwani kukaguwa shughuli za uchimbaji Madini na Mapato ya Serikali na Halmashauri katika Machimbo kwenye Kitongoji cha Nyandolwa, Kata ya Mwenge, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ameahidi kuwatibia Majeruhi wote walioko Hospitali mpaka watoke baada ya Sehemu ya Machimbo ya Mgodi huo kuanguka na Baadhi ya watu kujeruhiwa.
Akiongea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje, baada ya kutambulishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Nice R Munissy, aliwaambia wachimbaji hao kuwa haya ni mpenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa Baraza limeona lije liwape pole kutokana na yalotokea siku ya jana tarehe 15/09/2021 katika maeneo ya Machimbo baada ya baadhi ya Mashmo kuporomoka.
Alisistiza kuwa Baraza limeona lije liwaone ikiwa ni sehemu ya kazi yake ya kutatuwa changamoto za wananchi. " Halmashauri ni kiungo kati ya Wananchi na Serikali kuu, tumekuja kupata changamoto zenu na kwenda kuzifanyia kazi. kama zitatushinda basi tutaziwasilisha Serikali kuu" alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza Mwenyekiti wa Chama Wilaya ya Shinyanga, Mwenyekiti Alitowa kwanza pole na kusema wenyewe kama Chama cha Mapinduzi wameguswa sana na tukio hili, na kuwa walivosikia Mhe. Mbunge na waheshimiwa Madiwani wanakuja kuwapa pole basi wakaona nao wajiunge nao. " Tunatowa pole sana kwa Jamii ya Wachimbaji Nyandolwa". aliwaomba Wachimbaji kuchukuwa tahadhari zote zinazohitajika wakati wa Kuchimba na kutafuta Madini lakini akawatia moyo sana wananchi hao kuwa hiyo kazi haiwez kuachwa. "Mnafanya kazi nzuri sana na mnatupatia mapato,sio rahisi muache hii kazi bali ni muhimu tu kuchukuwa tahadhari zote zinazohitajika".
Akizungumza Mhe. Mbunge wa Jimbo la Solwa alianza kutowa salam za pole kwa kuwaambia wananchi hao kuwa baada ya kupata taarifa hii, aliamuwa kusitisha shughuli zake na kuja kuwapa pole wananchi. alisema tukio hili limeleta huzuni lakini tuko pamoja. alisema waliulizia kuwa kuna watu bado wanapata matibabu, akasema kwa hawa wanaopata matibabu yeye yuko tayari kuwahudumia mpaka wapate nafuu. aliwaahidi wachimbaji hao kuwa kwa kushirikiana na kamishna wa Madini mkoa wa Shinyanga, watahakikisha Eneo la Machimo la Nyandolwa linakuwa salama. swala la Usalama wenu ntalipeleka Wizarani, lazima muwe salama, mchape kazi kwa raha zenu.
Jambo la pili ni kama mnavoona, kuna uongozi wote kuanzia Mkurugenzi, Mwenyekiti wa Chama na wa Halmashauri, Madiwani wa Wataalam wote tumekuja hapa kuwapa pole. tunaendelea kufatilia tukio hili na usalama wenu, tutaendelea kufatilia mpaka pale tutapoona kuwa mnafanya kazi salama na kuwa mazingira yanaboreshwa ili mfanye kazi kwa Amani na utulivu. Mheshimiwa Mbunge alisema leo si siku ya kuongea mengi kwani bado watu tuna majonzi. kwa hayo machache alishukuru sana kupata fursa ya kuongea na wachimbaji na wafanyakazi wa migodini.
Akihitimisha Mazungumzo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi Nice alisema kwanza anawapongeza sana wachimbaji na wafanyakazi wa Mgodi kwa utulivu waliouonyesha kipindi cha matatizo ya kuporomoka kwa baadhi ya Mashimo ya Migodi, pili alimshukuru Mhe. Mbunge kwa kuamuwa kuwasaidia Majeruhi wote wa Mgodi na kuwashughulikia afya zao mpaka watakapopona kabisa.
Aliwashukuru sana Wachimbaji kwa kuwa tangu walivoachana jana jioni mpaka leo hajasikia vurugu zozote na watu wanaendelea kuchapa kazi kwenye maeneo ambayo ni salama. ila alitumia nafasi hiyo kwashukuru sana wananchi kwa weledi wao wa kuchaguwa Viongozi wasikivu. "mmeona shida imetokea jana tu lakini leo Viongozi wote wako tayari hapa nanyi. hii inaonyesha kwamba nyie ni wananchi makini ndio maana mkachaguwa Viongozi wasikivu na wenye Huruma."
Alihitimisha kwa kuwambia kuwa kwa Amani walioionyesha atawapa ushirikiano wote unaohitajika kama Mkurugenzi mwenye dhamana ya Halmashauri hii na kuwa atahakikisha changamoto zote zilizo ndani ya uwezo wetu kama Halmashauri zitatatuliwa kwa haraka na zile zilizo nje ya uwezo wetu tutashirikiana sana na Viongozi wa juu tuhakikishe zinatatuliwa kwa wakati. kwa kuwa bado kuna wasiwasi kuwa kuna wenzetu bado wako kwenye mashimo basi tuache mazungumzo haya ili kazi ya kuwatafuta wenzetu na masalia iendleee, aliwaoma wananchi hao kuwa Mungu awabariki sana na anawatakia kila la kheri kwenye shughuli zao.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.