Maagizo hayo yametolewa na mkuu wa wilaya ya shinya nga Mhe. Julius Mtatiro kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, uliofanyika 28-03-2024 katika kijiji cha Manyada, Kata ya Usanda.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya alisema waache kulima kwenye mashamba ya shule na kujitafutia mashamba yao binafsi . Mashmba ya Shule yalimwe na Wanafunzi kwa ajili ya kupata chakula wanapokuwa shuleni
“kuanzia leo nasitisha Mwalimu yeyote kulima kwenye mashamba ya shule” alisema Mhe. Mtatitro.
Aidha, Mhe. Mtatiro alisema ajenda ya wanafunzi kula shuleni haina mjadala na kuwataka wazazi wawe tayari kushirikiana na kamati ya shule na walimu kuhakikisha wanachangia chakula kwa ajiri ya watoto kula chakula shule na sio kwa madarasa ya mitihani tu bali ni wanafunzi wote.
Naya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. David Rwazo alisema utaratibu wa waanafunzi kula shuleni ni wakitafa na ni swala la lazima ili kuhakikisha watoto wanakuwa na lishe bora. Pia aliwataka walimu kutekeleza maagazo ya mhe. Mkuu wa Wilaya na kuahidi ofisi ya Mkurugenzi itasimamia utekelezaji huo.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Julius Mtatiro akizungumza na Wananchi wakati wa
Mkutano wa Hadhara
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.