Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Msingi Mhe. Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Katika Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Tarehe 15/1/2024.
Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi na kuhudhuliwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje, Wakuu wa Divisheni na Vitengo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Kisena Mabuba,Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Viongozi wa Dini na Waandishi wa Habari.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Msingi Mhe. Samizi akizungumza akatika Kikao hicho amepiga marufuku uuzaji wa Vyakula maeneo ya Shule kwa kipindi hiki cha mlipuko ya Magonjwa ya Kuhara na Kutapika na kuwataka Wazazi wachangie Chakula Shule ili Wanafunzi waweze pata chakula shuleni kilicho salama kwa afya zao.
Mhe. Samizi ameagiza taarifa zitolewe mara moja kwa Jamii kuhusu uwepo wa Ugonjwa wa Kipindupindu kupitia Vyombo vya Habari, Matangazo ya Barabarani, kwenye Mikutano ya Hadhara kama vikao kuanzia Ngazi ya Mtaa hadi Kata , Taasisi za Elimu na Taasisi za Dini.
Awali, Mkuu wa Wilaya alisema Magonjwa hayo ya mlipuko husababishiwa na mazingira mchafu, hivyo viongozi wanatikiwa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa masafi hasa maeneo ya huduma za Chakula na vyazo vya Maji ili kudhibiti Magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu.
Aidha, amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha Maeneo ya Masoko, Magulio na Minada kunakuwa na Vyoo bora na Maji safi tiririka ili kuepuka kusambaa kwa Magonjwa ya mlipuko ya kuhara na kutapika.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.