Mhe. Naibu Waziri wa Teknolojia Eng. Kundo jana tarehe 14/08/2021 amewasilisha Neema Mkoa wa Shinyanga.
kwanza alikabidhi Computer 30 na Printer 4 kwa shule za Sekondari ili ziweze kuunganishwa na Tehama. akikabidhi vifaa hivo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Philemon Sengati, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jacinta Mboneko, Mbunge wa Viti Malum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Eric na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Ndg NICE R. MUNISSY
Pili aliwasilisha Sh. 1.1 Billioni kwa Ajili ya Mradi wa Anuani za Makazi Mkoa wa Shinyanga. Akizungumza Mh Naibu Waziri, Alisema " Mhe. Rais anawapenda sana Shinyanga. ametuagiza tulete hiyo pesa kwa ajili ya Mradi wa Anuani za Makazi. jambo ambalo ameamuwa kulifanya Tanzania Nzima. " Leo namshukuru Mungu nimewafikishia Shinyanga na sasa ni kuona Fedha hizo zinatumika kama zilivopangiliwa na Serikali". Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Mhe. Mkuu wa Wilaya walitumia Fursa hiyo kuishukuru sana Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mama yetu Mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Neema hazikuishia hapo, Mhe. Naibu Waziri huyo aliwaambia Waheshimiwa Viongozi hao wa Mkoa na Wilaya kuwa pia Serikali imetowa fedha ya Ujenzi wa Minara 4 ya Mawasiliano ili kuweza kusogeza huduma za Mawasiliano karibu na Wananchi. Minara hiyo minne (4) Itajengwa Katika Mkoa wa Shinyanga ili kuwaletea wananchi wetu Maendeleo wanayoyahitaji. Hakika Swala la Mawasiliano ni muhimu sana na hatutaki wananchi wabaki nyuma kwenye matumizi ya Mawasiliano na Teknoljia ya Habari.
Pichani juu ni Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Philemon Sengati, Baada ya Ukaguzi wa Madarasa yatayofungwa Computer hizo, Akizungumza na Naibu Waziri wa Teknolojia Eng Kundo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.Jacinta huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. NICE akiwasilkiliza.
Kwa Niaba ya Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sengati Alisisitiza umakini wa Hali ya Juu utatumika kuhakikisha Miradi yote ya Serikali inatekelezwa kama ilivopangwa. aliahidi kuwa Mkoa umejipanga kutkeleza Miradi yote kama ilivopangwa na Serikali na watahakikisha Malengo tarajiwa yanapatikana kwa Ufanisi mkubwa. "Tutasimamia Miradi hii bila kumuonea aibu mtu yeyote atayetaka kuikwamisha, tutakuwa wakali hasa kuhakikisha Malengo yalokusudiwa yanafikiwa" Alisisitiza Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Naibu waziri Aliwashukuru Wenyeji wake na kuendelea na Ziara za Ukaguzi wa Miradi ya Serikali na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.