MAPATO NDIO MSINGI WA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashjauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Simon Berege afanya Kikao kazi na Waganga Wafawidhi na Wasaidizi wa Hesabu wa Vituo vya kutoa huduma ya Afya.
Kikao hicho kimefanyika Tarehe 18/8/2023, katika Ukumbi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, iliopo Makao Makuu ya Halmashauri Kata ya Iselamagazi.
Akiongea katika Kikao hicho, Mkurugenzi Berege ameeleza umuhimu wa ukusanyaji mapato sekta ya Afya na kuwataka Waganga Wafawidhi na Wasaidizi wa Hesabu kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuongeza mapato katika maeneo yao ya kazi.
Mkurugenzi Mtendaji amemuagiza Mganga Mkuuu wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga kuandaa mafunzo ya kuwajengea na kuwaongezea uwezo Wataalam wa Afya katika matumizi ya Mifumo ya mapato.
Aidha, Ndg Berege amewataka Wataalam hao kutoa huduma bora kwa kuzingatia Weledi, Taratibu, Kanuni za Utumishi wa Umma. Huku akisisitiza matumizi ya lugha nzuri na kuvaa sale za kazi wakati wakitoa huduma kwa Wagonjwa.
Ameongeza kwa kuwahimiza Wataalam hao kuzingatia usafi wa Mazingira katika maeneo yao ya kazi na muda wa kuanza kutoa kazi ni saa 1:30 Asubuhi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt Nuru Yunge , amehaidi kutekeleza maagizo yaliotolewa ili kuongeza ukusanyaji mapato divisheni ya afya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.