Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje amesema kuweka Fedha za Mapato Benki inasaidia katika usalama wa Fedha na kuondoa migigogoro baina ya Wananchi na Watendaji wa Kata na Vijiji. Aidha, ameagiza Akaunti zote za Benki za Vijiji zilizo kufa zihuishwe kuzitaka Kamati za maendeleo ya Kata (WDC) kutekeleza na kusimamia waraka huo.
Awali , akiwasilisha taarifa ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika Mkatano wa Baraza la Madiwani wa Kupokea na Kujadili taarifa za Kamati Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 uliofanyika Mei 10, 2024. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Stewart Makali aliwataka wakusanyaji wa mapato kuweka Fedha Benki na michango yote katika jamii kwa ajili ya maendeleo ya Kijiji iwekwe Benki.
Aidha, alieza kuweka fedha Benki ni kuzingatia Waraka Na. 1 wa hazina unaohusu utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2023/2024 na halmashauri ilitoa nakala ya Waraka kwa Viongozi na Watendaji ngazi ya Kata na Vijiji kama rejea.
“katika Waraka huo moja ya masuala yaliyoelezwa kuzingatiwa ni matumizi ya Mfumo katika makusanyo na matumizi ya Fedha zote katika nganzi zote ikiwemo Vijiji na Kata”. alisema Mwl. Makali
Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Fabian Kamoga alisema kwa mujibu wa muongozo ndani ya masaa 24 fedha zinatakiwa ziwekwe Benki baada ya kukusanya. Na kila inapofika tarehe 15 ya kila Mwezi waziri wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa atakuwa anatoa taarifa ya mapato kwenye Halmashauri zote Tanzania.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ngassa Mboje akizungumza wakati wa
Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na Kkujadili taarifa za Kamati
Kaimu Mkurugenzi akiwasilisha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Waheshimiwa Mdiwani wakichangia Mada wakati wa Mkutano wa Baraza
Kamati ya Usalama ya Wilaya na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupokea
na kujadili taarifa za Kamati
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.