Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5.
Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo.
Mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
“Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.
Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya afya.
Makamu wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto wa kike.
Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara amesisitiza Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.