Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. NICE R. MUNISSY leo tarehe 11/08/2021 amekabidhiwa Nyaraka Muhimu za Makabidhiano ya Ofisi na Mkurugenzi anayeondoka Bi. Hoja N. Mahiba kama Vitendea kazi vya Ofisi huku wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa S. Mboje.
Bi. Hoja Mahiba alimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama Nyenzo Muhimu ya Ufanyaji kazi. pia Alimkabidhi Taarifa za Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Shughuli za kila Idara na Vitengo. pia Alimkabidhi Taarifa muhimu ya Mali za Halmashauri mbele ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri.
Akizungumza kwenye Hafla hiyo, Mkurugenzi anayeondoka Bi. Hoja Mahiba Aliwashukuru sana Viongozi na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa ushirikiano waliompa na kuwaomba ushirikiano huo huo wampatie Bi NICE. "Ushirikiano huu mlionipa, umetusaidia kufanya makubwa, hasa kwenye kupandisha Mapato ya Halmashauri, Nawaombeni muuendeleze na Kumpatia Mkurugenzi wetu mteule alieingia"... Aliwasihi wafanyakazi kuwa kama kuna Madhaifu aliwatendea wakati wa Utendaji kazi wake basi anaomba wamsamehe sana na wajuwe kuwa hakuwa na nia mbaya bali ni utekelezaji wa Shughuli za Serikali.
Akiongea kwenye Makabidhiano hayo, Bi NICE Alisema " Mimi naamini sana kwenye "Team Work"" Alisisitiza. alisema yeye ni muamini sana wa Haki, aliwaomba wafanyakazi kufanya kazi kwa Bidii na kuwa wabunifu. :"Napenda sana 'Creativity' Idara na Vitengo ningependa sana nione creativity. alisisitiza Mkurugenzi huyo Kijana. Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndugu Muhochi Fredy Mweka, pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo.
Mhe. Ngassa S. Mboje akizungumza kwenye Makabidhiano hayo, Alisisitiza kuwa Bi Hoja alikuwa Kiongozi wa Aina yake, mwerevu, msikivu, hakuwa mtu wa kujikweza, Mwenye kumheshimu kila mtu, alisisitiza kuwa Alijenga Mahusiano mazuri kati ya Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wakiwemo wabunge, wakuu wa Wilaya na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama. "kwa kweli kwenye Jambo Hoja alifanikiwa sana ni kujenga mashirikiano na Masikilizano kati ya Viongozi, madiwani na wataalam" Tumekuwa kitu kimoja kwa muda wote alipokuwa hapa". hakupenda kusikia migogoro na hivo aliishughulikia mapema kwa kuzungumza na wadau wote migogoro inapotokea. alimuomba Bi NICE kufata nyayo za Mtangulizi wake kwenye kuendesha hii Halmashauri. mheshimiwa Mwenyekiti mara kwa mara alionekana kukatiza Hotuba yake hali wengi waliitasiri kama Majonzi kushindwa kuhimili kuona Bi. Hoja akiondoka.
Akimsaidia, Mh Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mh Isaack M Sengerema, kumalizia Hotuba yake,,alisisitiza kuwa wanamuomba sana Mwenyezi Mungu kuwa moyo aliokuwa nao Bi Hoja ndio huo huo awe nao Bi NICE, Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mh Sengerema alisisitiza kuwa hata Jamii ya wana Iselamagazi (Ambapo yeye ni Diwani) kwa muda wa Miaka miwili sasa tangu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ihamie Iselamagazi, Jamii imekuwa Ikiona mchango wa Mkurugenzi anayeondoka kwenye Shughuli za Kijamii hasa Misiba, Harusi na Shughuli za Kidini. mara zote. "Bi Hoja amekuwa mstari wa mbele kujihusisha na shughuli za wananchi wa Eneo la Iselamagazi kitu ambach Jamii hii itamkumbuka sana".
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.