Halmashauri ya Wialaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Mama O Daries yatoa mafunzo kwa wafugaji kutoka Kata ya Tinde, Didia, Nyida, Puni na Usule. Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mhe. Luhende Masele Diwani Kata ya Didia.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwazesha wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa na kupelekea kuongezeka kwa UZALISHAJI na upatikanaji wa maziwa.
Akifungua mafunzo hayo mhe. Masele alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wafugaji kujiwezesha kiuchumi. Nawasii wafugaji watumie maarifa watakayoyapata kwenye mafunzo haya na kuyafanyia kazi.
Aidha, mhe. Masele alisema baadhi ya wafugaji wamekuwa hawazingatii kanuni za ufugaji bora kama vile kuosha mifugo, kuchanja mifugo, kujenga mazizi bora, kuwapatia lishe bora pamoja na kuwa na idadi kubwa ya ng'ombe katika eneo dogo. Hali hiyo hupelekea upatikanaji wa maziwa pamoja na mazao mengine yatokanayo na Ng'ombe kuwa hafifu.
“ wataalam wa mifugo wa Halmashauri wapo na wana Elimu na ujuzi tuwatumie ipasavyo na wakileta chanjo kwa ajili ya Mifugo tuhakikishe tunapeleka ng’ombe ili kuwakinga na magonjwa. Tukizingatia haya uzalishaji wa maziwa utaongezeka na tutainuka kiuchumi" alisema Mhe. Masele.
Awali, Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Mtaalam wa Mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Dkt Isaya Gabiriel alisema, iliNg’ombe aweze kutoa Maziwa kwa wingi ni lazima awe na Afya bora. Hivyo ni lazima Mfugaji azingatie Chanjo,, Matunzo bora,Tiba, Uogeshaji na Uvyuvyiziaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mama O Daries Bi. Thabitha Gityamwi aliwataka wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa huku wakifanya kazi kwa ukaribu na wataalamu wa mifugo na kuzingatia ushauri wanaotoa ili kuongeza upatikanaji wa maziwa na kukuza kipato kwa wafugaji. Bi. Thabitha alieza jinsi kampuni yake itakavyofanya kazi na Wafugaji hao na Kutoa Soko la uhakika la maziwa, kampuni ya hiyo itanunua kila lita moja ya maziwa kwa sh. 1000.
Mhe. Luhende Masele, Diwani wa Kata ya Didia akizungumza wakati wa
mafunzo kwa wafugaji.
Dkt. Isaya Gabiriel akitoa mafunzo kwa Wafugaji
Mfugaji kutoka Kata ya Tinde Bw. Manyesha Shilatu akichangia Mada wakati
ya Mafunzo.
Mfugaji kutoka Kata ya Nyida Bi. Marija Mbata akizungumza wakati wa mafunzo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mama O Daries akielezea jinsi kampuni yake
itafanya kazi na wafugaji hao.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi Mhe. Luhende Masele , Wataalam kutoka
Halmashauri, Mkurugenzi wa Mama O Daries na Wafugaji baada ya Mfunzo.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.