Wataalamu kutoka Tume ya maadili wametoa mafunzo ya uwajibikaji wa pamoja kwa Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Mafunzo hayo yamefanyika leo 07 Februari, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri .
Mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha Waheshimiwa Madiwani namna ya uwajibikaji wa pamoja katika utendaji kazi ambao unamtaka kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kufanikisha malengo ya Halmashauri.
Aidha, mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo amesema kuwa uwajibikaji wa pamoja ni kuwa na kauli moja na kusimamia maamuzi yaliyofikiwa kwa pamoja, kufuata sera, sheria na kanuni wakati wa kufanya maamuzi.
Akichangia mada, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba ameishukuru Tume ya Maadili ya Viongozi kwa mafunzo mazuri na yenye tija “ ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatatusaidia sisi wataalamu pamoja na waheshimiwa madiwani kufanya kazi tukiwa timu moja na kutatua changamoto za Wananchi”
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje, akifunga mafunzo hayo amewasisiitiza Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kufanya kazi kwa ushirikiano kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa shughuli za halmashauri ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi, ulinzi na usalama.
Afisa maadili kutoka Tume ya maadili, Bw. Amasha Bura akiwasilisha mada
ya uwajibikaji kwa pamoja
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia mada
Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Said Kitinga akichangaia mada wakati wa mafunzo
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.