Mnamo tarehe 01.05.2018, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga iliendesha mafunzo ya mfumo wa mapato katika ukumbi wa Halmashauri,mafunzo hayo yakijumuisha Wakuu wa Idara na Vitengo .Malengo ya kuanzishwa kwa mafunzo hayo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo ilikuwa ni pamoja na
Ufanyaji Kazi wa Mfumo
Pia,walielekezwa ufanyaji kazi wa mfumo ili kuhakikisha ufanisi wa ukusanyaji unakuwepo
MAMBO YA KUZINGATIA KWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO WAKATI WA UKAGUZI
AINA ZA VYANZO VYA MAKUSANYO KWENYE MFUMO
Walielekezwa aina 2 za vyanzo vya makusanyo
CHANZO KUTOKANA NA MTEJA ASIYE WA KUDUMU
Chanzo hiki huitwa (Miscellaneous Sources) mara nyingi mteja wake si wa kudumu , hawa watalipa kwa mkataji wa ushuru kwa kutumia POS na baadae mkata ushuru atafuata bill ya wote aliowakatishia ushuru kwa ujumla wake na kwenda kuwasilisha fedha benki halafu atapeleka deposit slip kwa mtunza fedha na kupewa stakabadhi.Mfano wa vyanzo vya Missellenous Sources ni pamoja na ushuru wa minada,ushuru wa soko au Vizimba
CHANZO KUTOKANA NA MTEJA WA KUDUMU
Chanzo hiki huitwa' Main Source' maana yake mteja mwenyewe ndiye hufika Halmashauri na kuchukua bill yake ambayo ataenda nayo benki kwa ajili ya kufanya malipo ya fedha.Mfano wa chanzo hiki ni pamoja na:- Property Tax,House Rent,hotel levy ,business license.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.