Wataalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga na Kituo cha Afya cha Nindo wamepatiwa mafunzo ya kumsaidia mtoto kupumua yakiwa na lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Mkoa kupitia mradi wa USAID AFYA YANGU. Mafunzo yametolewa na Daktari Mbobezi wa Watoto, Dkt.Yustina Treba kutoka Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kwa muda wa siku mbili Februari 26-27, 2024 na yamefanyika kwa nyakati tofauti katika Hospitali ya Wilaya na Kituo cha Afya cha Nindo.
Daktari Mbobezi wa Watoto, Dkt.Yustina Treba kutoka Hospitali ya Mkoa wa
Shinyanga akifundisha kwa vitendo jinsi ya kumsaidia mtoto mchanga kupumua
Baadhi ya Wataalamu wa Afya wakifuatilia kwa makini wakati wa mafunzo.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.