• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework
Government Web Framework

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwongozo wa Tovuti za Serikali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Usafi na Manzingira
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki na Misitu
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Mipango
      • Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Elimu , Afya na Maji
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
    • Madiwani wa Kuchaguliwa
    • Madiwani wa Kuteuliwa
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Majarida
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Kanzi Data ya Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Video

mafunzo kwa watumishi wa umma juu ya kutumia planrep na FFARS

Posted on: September 28th, 2017

Mkurugenzi wa Wilaya   amefungua mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa Mipango na Bajet (Planrep) pamoja na mfumo wa  uhasibu na utoaji taarifa unaojulikana kwa Kiingereza kama  (FFARS - Facility Financial Accounting and Reporting System). Mfumo huu wa kielektroniki unasaidia utekelezaji wa utoaji wa rasilimali fedha moja kwa moja kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma kwa kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma.  "FFARS itawapatia  watoa huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawezesha kutunza taarifa za kifedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vya kutolea huduma.  FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa. Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, kwa jamii. Alisema Mkurugenzi wa Wilaya.

Kuanzia Julai 1, 2017 Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iliaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma  kwa ngazi za Halmashauri.  Vituo vya kutolea huduma ambavyo vinapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya.  Zoezi hili ni sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Mfumo huu mpya wa kupatiwa Rasilimali Fedha unatoa motisha kwa vituo vya kutolea huduma  na kuongeza kipaumbele cha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuongeza usawa na uwazi.  Upelekaji wa Rasilimali Fedha moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma inahakikisha kuwa Fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa. Mkakati huu mpya wa kuboresha sekta ya afya  na elimu ni msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta za Umma (PS3).

Mafunzo ya Mfumo wa FFARS yamekusudia kuwawezesha watumishi katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa FFARS ambao ndio watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS katika  Vituo vya Afya, Zahanati na Shule za Msingi na Sekondari za Wilaya  ya Shinyanga. Mafunzo haya yatahakikisha kuwa watoa huduma katika vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa fedha na kutoa  huduma bora kwa wananchi wote .

Mfumo huu wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID.  Mfumo utatumika katika vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na shule, na uhuishaji huu wa mfumo utarahisishia na kuongeza ufanisi katika mifumo ya Serikali ya Tanzania na kuboresha usimamizi na matumizi ya Rasilimali za umma.

Pamoja na mafunzo ya FFARS, pia watumishi watajifunza mfumo mpya na ulioboreshwa wa kupanga bajeti unaojulikana Planing and Reporting (PlanRep) ambao utaanza kutumika kuandaa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019. Mfumo huu utapunguza gharama zilizokuwepo wakati wa uandaaji wa bajeti ya Halmashauri kama vile gharama za kutengeza vitabu vya bajeti, gharama za usafiri wa kupeleka bajeti katika ngazi ya mkoa na Wizarani. Kwa maana mfumo utaruhusu uandaaji wa bajeti na utumaji wa bajeti kielektroniki kutoka ngazi ya kutolea huduma hadi wizarani bila kuhitaji watumishi kusafiri.

Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni wa miaka mitano na unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara.  PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 09, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA ( MCHUJO) KADA YA DEREVA DARAJA LA II April 15, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA TATU April 17, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI April 19, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MITI 1000 YAPANDWA KATA YA SALAWE KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU.

    December 09, 2024
  • BABA BORA, SAUTI YA UMMA NA WANAWAKE VIONGOZI WAPATIWA VITENDEA KAZI

    November 15, 2024
  • WANADIDIA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI NOVEMBA 27, KUPIGA KURA

    November 15, 2024
  • MASHINE YA X-RAY MBIONI KUFIKA KITUO CHA AFYA TINDE

    November 15, 2024
  • Tazama zote

Video

wiki ya maji
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Muundo wa Taasisi
  • Muundo wa Taasisi
  • Video mbali mbali
  • Historia
  • Fomu ya Likizo
  • Leseni ya Makazi
  • Fomu ya Mkazi wa Ardhi kulipwa fidia

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • ofisi ya taifa ya takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    NIndo - Iselamagazi

    Anuani ya posta: 113 Shinyanga

    Simu: 0282-986382

    Simu: 0282-986382

    Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.