Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Februari, 2024 limeridhia na kumepitisha Mpango na Bajeti ya Tsh. Billion 40.5 kwa mwaka 2024/2025. Maamuzi hayo yamefanyika wakati wa mkutano maalumu wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri . Fedha hizo zitatumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali za utoaji huduma, utawala na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri , Afisa Mipango, Bw. Mathew Kayanda ameeleza kuwa bajeti hiyo imezingatia miongozo ya kitaifa na halmashauri. Miongozo hiyo ni pamoja na kupokea mapendekezo kutoka kwa wajumbe mbali mbali katika ngazi ya Wilaya, Kata, Vijiji, Vitengo na Divisheni za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga .
Aidha, Bw. Kayanda amefafanua kwamba katika rasimu hiyo ya Bajeti , kiasi cha Bilioni 3.4 ni fedha zitatokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri, kiasi cha shilingi Bilioni 24.9 ni ruzuku ya mishahara ya Watumishi, kiasi cha shilingi milioni 1.2 ni ruzuku ya uendeshaji wa ofisi ( OC) na kiasi cha Bilioni 10.4 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali kuu na wahisani.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri katika hotuba yake amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmasahuri ya Wilaya ya Shinyanga kuendeleza jitihada alizozianzisha katika kutekeleza majukumu ya halmashauri na kumtaka kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati ili wananchi wafurahie matunda ya nchi yao. .... “ nina imani kubwa na wewe na sina mashaka na utendaji kazi wako” amesema Mweyekiti
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wakati wa kujibu mbalimbali, Mkurugenzi amesema amebaini kuwa vyanzo vingi vya mapato haviwekwi kwa uhalisia na hata vinavyowekwa havifikii malengo. Hivyo, amewaomba Waheshimiwa Madiwani na kuwataka watendaji wa halmashauri kuwa kitu kimoja na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta maendeleo kwa wananchi. “.....pale ambapo hatufanyi vizuri tuambiwe pasipo kuoneana haya na tunapokosea tukosolewe kwa staha kwa kuwa wote tunaijenga halmashauri moja’....ameeleza Mkurugenzi Mtendaji.
Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Ngassa Mboje akifungua kikao cha Baraza
la maalumu la kujadili na kupitisha rasimu ya Mpango na bajeti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg. Kisena Mabuba
akichangia mada wakati wa kikao cha baraza maalumu la madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mpango na bajeti ya 2024/2025.
Wajumbe wa kikao cha Baraza maalum la waheshimiwa Madiwani
Wakichangia mada.
Kamati ya Usalama ya Wilaya na Wataalamu wa Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.