Mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024 umefanyika Machi 7, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka Kamati za Kudumu. Kamati hizo ni Kamati ya Fedha Uongozi na Mipanga, Kamati ya Afya, Elimu na Maji, Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Maadili na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi.
Akizungumza wakati wa kufungua Baraza hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe.Nicodemus L.Simon ambaye ni Diwani wa Kata ya Masengwa ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Aidha, akiwasilisha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Dkt Nuru Yunge amesema Halmashauri imepokea fedha kiasi cha Sh. 541,800,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali katika sekta ya Elimu, Afya, Maji na huduma nyingine za Jamii kwa kipindi cha robo ya pili.
“Natoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri fedha hizi kwa kuwa zitasaidia kwa sehemu kubwa kupunguza uhaba wa miundombinu ya elimu,” alishukuru Dkt. Yunge.
Akiwakilisha taarifa ya Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Diwani wa Kata ya Didia Mhe. Luhende P Masele alieleza kuwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024, kamati imetembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na ameipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa inayoifanya katika halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Nidodemus L. Simon akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani
kujadili taarifa za Kamati za Kudumu katika mkutano wa Baraza la
Madiwani katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Nuru Yunge akiwakilisha taarifa ya
Mkurugenzi Mtendaji wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani
Mhe. Luhende Masale, Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo katika kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha
2023/2024 kutoka Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kwa niaba ya
Mwenyekiti wa Kamati.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Elimu na Maji Mhe. Isack Sengelema,
ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Iselamagazi akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo ya Pili kwa
mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka Kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
Mhe. Sonya J. Mhela, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Itwangi
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika
kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mjumbe wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi, Mhe. Susana N. Malembela
ambaye ni Diwani Viti Maalum akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa
fedha 2023/2024 kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.