Timu ya Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imewasili leo Juni 17,2024 katika hospital ya
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na imeshaanza kutoa huduma kwa wakazi wa Halmashauri hiyo.
Huduma za kibingwa zimeanza kutolewa leo Juni 17 hadi Juni 22, 2024. Huduma zinazotolewa ni pamoja na
huduma za afya kwa watoto, afya ya uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake, magonjwa ya ndani
( shinikizo la damu, kisukari n.k), upasuaji na huduma za ganzi na usingizi.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya madaktari hao yaliyofanyika mkoani Shinyanga, Mratibu wa Timu hiyo
ya Madaktari Bingwa Dkt. Everine Maziku kutoka Idara ya Afya,Uzazi,Mama na Mtoto Wizara ya Afya amesema
mkoa wa Shinyanga umepokea Madaktari 30 ambao watatoa huduma za kibingwa katika halmashauri zote za mkoa huo.
Kwa upande wao wakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga waliofika hospitalini hapo, wamemshukuru Rais Samia
kwa kuwaletea Madaktari Bingwa kwa kuwa anawajali wananchi wake kwa kuhakikisha wanaendelea kuwa na afya njema.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.