Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imehuisha mabaraza na madawati ya watoto 58 katika shule 46 za msingi
na shule 12 za sekondari ikiwa ni hatua muhimu katika malezi, ulinzi , makuzi na maendeleo ya mtoto.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Bw. Joseph E. Ntomela wakati akitoa taarifa
ya shughuli zilizofanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yanaadhimishwa tarehe 16
Juni kila mwaka.Mabaraza ya Watoto ni jukwaa pekee la watoto lilianzishwa na Serikali kwa lengo la kuwashirikisha
watoto katika kujadili na kutoa maoni yao katika masuala yanayowahusu. Jukwaa hili linalotumika katika kuwaelimisha
watoto masuala mbalimbali yanayohusu maisha yao ya sasa na baadaye nje ya mfumo rasmi wa elimu, ikiwa pamoja na
uongozi, uadilifu, uzalendo kwa Taifa lao na masuala mengine mtambuka ikiwa pamoja na VVU na UKIMWI, mazingira, stadi
za kazi na usawa wa Kijinsia.
Mabaraza ya Watoto yanaimarisha uwezo wa Watoto katika kujitambua, kujiamini, kujieleza na
kujilinda dhidi ya ukatili wa aina mbalimbali.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.