Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Edward Maduhu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amegawa vishkwambi na sare maalum ikiwa ni vitendea kazi kwa Maafisa Kilimo ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Ndg. Maduhu amesema vishikwambi hivyo vitakuwa na uwezo wa kumrahisishia Afisa Kilimo kwa kutoa taarifa za kila Wiki, Mwezi na Mwaka ambapo kifaa hicho kinaunganishwa na mifumo ya utendaji kazi kama ARDS, M-Kilimo na Mfumo wa Mbolea hivyo atatoa taarifa ili ziweze kutumwa Mkoani na Wizarani.
Aidha, amewakumbusha Maafisa Kilimo kwenda kutoa elimu ya upimaji udongo na kuwasaidia kuchukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara ya kitaalamu inayopatikana katika Ofisi za kilimo za Halmashauri. Elimu ya upimaji udobgo itamsaidia mkulima kufahamu shamba lake linaitaji mbolea kiasi gani ili aweze kuongeza tija katika uzalishaji wake.
Wakizungumza baada ya kupokea vishkwambi Ndg. Gabaruda Kidaweda ,Afisa Kilimo kata ya Mwenge na Bi. Odetha Ngimbo Afisa kilimo kata ya Salawe wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya kilimo na kuondokana na ripoti za makaratasi lakini pia vazi rasmi litawatambulisha kwa wateja kirahisi.
Ugawaji wa vishikwambi kwa Maafisa Kilimo ni mpango wa Wizara ya Kilimo chini ya Waziri mwenye dhamana Mhe,. Hussein Bashe kusaidia maafisa kuweza kuwahudumia wakulima kwa urahisi na kuongeza tija katika ustawishaji wa mazao.
BAADHI YA MAAFISA KILIMO KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUPOKEA
SARE NA VISHKWAMBI.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.