Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanajishughulisha na masuala ya kutetea haki za wanawake , vijana na watoto,wameadhimisha siku ya mtoto wa Afika duniani.Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Singita iliyopo katika kata ya Usanda, aidha kimkoa maadhimisho hayo yatafanyika June 16 wilayani Kahama.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu "Mtoto ni msingi wa taifa endelevu , Tumtunze ,Tumlinde , na Kumuendeleza."
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Bi. Christina Bukori , akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko , amewataka wazazi kutumia maadhimisho hayo kuacha vitendo vya kiukatili kwa watoto wao , aidha wanatakiwa kuwalinda pamoja na kuwatimizia mahitaji yao muhimu ili kutimiza ndoto zao.
Afisa ustawi Wilaya Bw. Deus Mhoja akitoa neno siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika kata ya Usanda wilyani Shinyanga.
Kikundi cha kwaya ya Agape kutoka shule ya msingi Singita kikitumbuiza kwaya yenye ujumbe wa kuwalinda watoto siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika duniani.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.