Na Monica Mnanka, Shinyanga DC
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 19, 2024 katika viwanja
vya Shule ya Msingi Didia, Kata ya Didia.
Katika maadhimisho hayo, mgeni wa heshima alikuwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Shinyanga,
Bi. Rehema Edson ambaye ameongoza mdahalo wa watoto kuhusu haki za mtoto kwenye maeneo ya haki
ya kulindwa, haki ya kushiriki, haki ya kutobaguliwa, haki ya kutonyanyaswa, haki ya kushiriki kutoa maoni
na haki ya kuendelezwa.
Aidha, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza shughuli zake katika halmashauri ya Shinyanga
yameshiriki kutoa elimu ya kuwajengea wananchi uwezo wa kupinga ukatili wa kijinsia.
Vile vile, imetoa elimu ya stadi za maisha na ushirikishwaji wa watoto wenye ulemavu kupata haki zote
za msingi. Mashirika hayo yaliyoshiriki ni pamoja na shirika la Pasheshi, TAI, THUBUTU, YAWE, GCI,
SHEDEPHA, TCRS na SHAI EVAC.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika duniani huadhimishwa kila tarehe 16 Juni.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.